- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
NYAMA YA MBUZI KWA MAPISHI TOFAUTI
Mahitaji
- Nyama ya mbuzi – kilo 1
- Vitunguu maji vikubwa - 2.
- Nyanya za kawaida - 6 (ukipenda unaweza nunua na ya kopo).
- Kitunguu swaumu - 1
- Tangawizi
- Karoti
- Hoho
- Kolimaua
- Njegere
- Mafuta
- Chumvi
- Maji
- Bizari
Maelekezo
- Katakata nyama, osha kisha weka vitunguu swaumu na tangawizi. Ache nyama pembeni kama nusu saa ili viungo viingie vizuri.
- Andaa karoti, vitunguu, nyanya, kwa kukata vipande vidogo vidogo.
- Menya viazi, osha, kata vipande vidogo kisha hifadhi kwenye sufuria ya maji ili visibadilike rangi.
- Andaa tangaziwi, vitunguu swaumu kwa kukata na kisha kuponda kwenye kinu
- Bandika mafuta yakichemka tia vitunguu maji vyote vikaange mpaka viwe vinakaribia kubadilika rangi
- Weka nyama ya mbuzi huku unaendelea kukoroga
- Weka chumvi, koroga ili ichanganyike vizuri.
- Weka pilipili hoho, carrots, kolimaua na njegere. Koroga kwa takribani dakika tano.
- Weka nyanya koroga kiasi na kisha funika na mfuniko.
- Mchanganyiko ukiiva weka nyanya ya kopo na maji kiasi ili kuivisha nyama.
- Weka viazi ili vipate kuiva na mchanganyiko wa nyama.
- Ili kuongeza ladha, weka bizari (au kiungo chochote cha kuongeza ladha ya chakula).
- Funika nyama yako kwa muda wa dakika ishirini.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment